SHAIRI: MABADILIKO YA TABIANCHI

Na Oscar Munga

Mabadiliko ya tabianchi,ni janga la dunia,
Vijana tusipofikiri hili,itatufikisha pabaya,
Matatizo yake nimengi,na bado hatujajifunza,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

Mengi matatizo yametokea,mabadilko kutuumiza,
Tukianzia kiataifa na bara,hata ulimwengu pia,
Ni vigumu kuzuia,wakati bado hatujafikiri,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

Njaa inaongezeka ,kwa masikini wasonakosa,
Wachache wanajikwamua,kuendesha yao maisha,
Wengi twaumia, hatuna pa kijishika,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

Mifugo nayo yaangamia,maji nayo hakuna,
Wafugaji walalamika,hakuna anayewasikiliza,
Yote kukosa maarifa,tabianchi kutokuijua,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

Mavuno nayo madogo,wakulima kukosa namna,
Halijoto kuongezeka,mimea pia hudumaa,
Nguvukazi ni vijana,tatizo ni maarifa,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

Wengi tunaoumia sana,ni sisi waafrika,
Wetu umasikini fikra,nayo teknolojia changa,
Ndio chanzo cha maafa,angali rasilimali twajivunia,
Vijana tusimame,mabadilko kuyakabili.

Vijana tuamke sasa,kulinusuru letu Taifa,
Tusambaze mengi maarifa,nazo mbinu za kisasa,
Wafugaji na wakulima,nao kuelimishwa,
Vijana tusimame,mabadiliko kuyakabili.

No comments:

Post a Comment